Habari ya uzima Viongozi,

Mimi niko salama kabisa, namshukuru Mungu. Napenda kuwakumbusha kuwa tulikuwa na mwaliko wa Wizara ya Afya chini ya RehabHealth kwenda kwenye kikao kilichofanyika tarehe 18 na 19 mwezi huu. Aliyetakiwa kufika kwenye kikao ni Mwenyekiti Mtendaji wa PHYSIOPLANET, ambaye ni mimi.

Leo nawapa taarifa rasmi kuwa sikufanikiwa kufika katika mwaliko huu kutokana na ukosefu wa ada na hela ya kujikimu. Tatizo hili limepelekea mimi kushindwa kufikisha mawazo yangu mazuri na ya kujenga nchi yetu upande wa afya. Kitu hiki kimeniuma binafsi kwani nilitamani sana kuchangia hoja za kujenga Wizara ya Afya.

Yote kwa yote ni kwa sababu ya chama chetu kutokuwa na mfuko wa kujiendesha na kutegemea wadau. Pamoja na hivyo, mhasibu aliweka jitihada za kuwaomba wanachama kuchangia lakini hakuna aliyejitokeza. Hili limekuwa jambo la kushangaza kidogo ukilinganisha na kazi zinazofanywa na viongozi wa PHYSIOPLANET tena bure pasipo na malipo yoyote, lakini tumeweza kuleta umoja mkubwa kati ya sekta moja ya afya na nyingine hata ushirikiano wa kimataifa.

Hivyo basi, napenda kuwaomba viongozi wenzangu kutokata tamaa hata sekunde moja kwani kazi ya afya ni wito. Nawaomba pia wanachama kuendelea kutupa ushirikiano wa dhati ili tuweze kujenga jamii bora yenye afya bora.

Pamoja na hivyo, nawashukuru sana wanachama kwa ushirikiano wenu. Mpaka sasa mmeifanya taasisi ya PHYSIOPLANET kuwa kubwa nchini Tanzania na chama pekee chenye watu wengi zaidi upande wa rehabilitation. Lakini pia napenda kuwataarifu kuwa baada ya kikao kuisha, niliwasiliana na Mkurugenzi wa REHAB HEALTH na kumweleza juu ya changamoto ya sisi kushindwa kushiriki kikao. Alitoa pole kwa taasisi na kutukaribisha tena mwakani kwenye kikao kijacho tena kuanzia maandalizi ya kikao.

Hivyo, tunaendelea kudumisha umoja na ushirikiano na REHAB HEALTH na taasisi zingine zenye nia njema juu ya nchi yetu na sekta ya afya kwa ujumla.

Ahsanteni sana. Nawatakia kila la kheri. Afya bora, jamii bora.

Amos Paschal
PHYSIOPLANET - CEO
+255626371854
ceo@amoleck.co.tz